YANGA MIKONONI MWA IHEFU

BAADA ya kusepa na pointi tatu mbele ya Mbeya City,Novemba 26,2022 Uwanja wa Mkapa kituo kinachofuata ni Highland Estate.

Yanga ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City na mtupiaji wa mabao yote mawili alikuwa ni Fiston Mayele ambaye anafikisha mabao 10.

Mayele alipachika bao la uongozi kwa pasi ya Khalid Aucho na lile bao la pili alipachika kipindi cha pili kwa pasi ya Jesus Moloko.

Kwa mujibu wa Ally Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa kazi inaanza kwa ajili ya kufikia malengo yao ya kutwaa ubingwa wa ligi.

“Tunajua wapinzani wetu Ihefu ni timu bora na ina wachezaji wazuri licha ya kutokuwa na matokeo mazuri lakini tunawaheshimu wapinzani wetu.

“Kikubwa ni kuona kwamba tunapata matokeo mazuri na kuendelea kukusanya pointi tatu kwani hilo ni jambo la muhimu,” .