>

AZAM FC KUIKABILI COASTAL UNION

KIKOSI cha Azam FC kinachonolewa na Kaimu Kocha Mkuu, Kali Ongala leo kitakuwa na kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Coastal Union.

Azam FC imetoka kushinda bao 1-0 dhidi ya Namungo FC na imekuwa kwenye kasi bora ndani ya ligi kwa mechi za hivi karibuni.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex saa 1:00 ambapo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Azam FC baada ya kucheza mechi 13 imekusanya pointi 29 inakutana na Coastal Union yenye pointi 12 baada ya kucheza mechi 11.

Ongala amesema anatambua mchezo utakuwa mgumu lakini wapo tayari kwa ajili ya ushindani.