NOVEMBA 26,2022 Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Simba, Boniface Lyamwike ametangaza rasmi siku ya uchaguzi mkuu wa Simba kwenye nfasi mbalimbali.
Lyamwike amesema:-“Nawatangazia wanachama wa Simba, wapenzi na mashabiki kwamba tarehe ya uchaguzi wa Simba itakuwa ni tarehe 29 Januari, 2023.
“Mwaka huu kanuni ambazo zitatumika kwenye uchaguzi wa Simba ni kanuni za Simba Sports Club. Huko nyumba tulikuwa tunatumia kanuni za TFF, katiba ya Simba ilikuwa inaruhusu..
“Kanuni ya sita (kanuni za uchaguzi Simba), kigezo cha kwanza mgombea lazima awe mwadilifu na awe na kiwango cha juu cha uaminifu. La pili lazima awe mwanachama hai wa klabu.
“Mtu yeyote ambaye anagombea nafasi ya mwenyekiti wa klabu ni lazima awe na angalau shahada ya chuo kikuu, na lazima awe na uwezo na haiba ya kuwakilisha klabu ndani na nje ya nchi.
“Anayegombea nafasi ya ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi lazima awe amefika kidato cha nne na cheti za kuhitimu, kigezo kingine awe mzoefu uliothibitishwa wa angalau miaka mitatu ya uongozi wa mpira wa miguu.
“Kingine asiwe amepatikana kamwe ya hatia ya kosa ya jinai, lakini pia angalau awe na miaka 25 na si zaidi ya miaka 64, lakini pia asiwe mmiliki, mwanahisa au kiongozi wa timu ngyine ya mpira wa miguu.
“Nafasi ambazo zitagombewa ni mwenyekiti nafasi moja, kutakuwa na mjumbe wa pili lakini pia kutakuwa na wajumbe wengine wanne. Jumla zitakuwa nafasi sita.
“Katiba inampa nafasi mwenyekiti atakayechaguliwa kuchagua wajumbe wengine wawili. Lakini pia kuna kigezo cha msingi sana, katika nafasi nne, angalau mmoja au zaidi awe mwanamke,” amesema.