KIUNGO WA KAZI YANGA KUIWAHI MBEYA CITY

KIUNGO wa kazi ndani ya kikosi cha Yanga, Aziz KI anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaoivaa Mbeya City kwenye mchezo ujao wa ligi.

Aziz KI alikosekana kwenye mechi tatu baada ya kufungiwa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB) kwa kosa la kukwepa kusalimiana na wachezaji wa timu pinzani.

Ilikuwa kwenye Kariakoo Dabi iliyochezwa Uwanja wa Mkapa, Oktoba 23 na ubao ukasoma Yanga 1-1 Simba ambapo bao la Yanga alifunga yeye mwenyewe Aziz KI kwa pigo la faulo huku kwa upande wa Simba Chama alimpa pasi Augustino Okra.

Mbali na kukosekana kwenye dakika hizo 270 laki tano ilikuwa faini kwa kosa hilo ni mchezo dhidi ya Kagera Sugar 0-1 Yanga, Yanga 4-1Singida Big Stars pamoja na ule uliotarajiwa kuchezwa jana dhidi ya Dodoma Jiji.

Hivyo Novemba 26 dhidi ya Mbeya City mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya staa huyo atakuwa miongoni mwa kikosi.

Kocha msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema:“Aziz KI anakosekana kwa kuwa amefungiwa hivyo akimaliza adhabu yake tunaamini atakuwa sehemu ya kikosi kwani uwezo wake unajulikana,”.

Kwenye ligi Aziz KI kacheza mechi 7 kayeyusha dakika 468 kafunga mabao mawili na ana pasi moja ya bao.