>

AZAM FC YAIVUTIA KASI COASTAL UNION

BAADA ya kumalizana na Namungo ugenini sasa kikosi cha Azam FC kinafanya maandalizi kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union.

Chini ya Kaimu Kocha Kali Ongala timu hiyo imetoka kupata ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Edward Manyama akitumia pasi ya Ayoub Lyanga.

Mchezo wa kwanza kwa Ongala kuwa benchi ilikuwa dhidi ya Simba uliochezwa Uwanja wa Mkapa ambapo waliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Mtupiaji kwenye mchezo huo alikuwa ni Prince Dube ambaye alitumia vema krosi ya kiungo James Akamiko.

Ongala ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo wao dhidi ya Coastal Union ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.

“Tunajua kwamba mchezo utakuwa mgumu lakini tupo tayari kwa ajili ya kupata matokeo chanya.

“Kila mchezaji anatambua wajibu wake na ninawapongeza kwa kuwa wamekuwa wakifanya kazi kubwa na hili ni muhimu kwetu kuendelea kupata matokeo mazuri,”.

Azam FC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 29 baada ya kucheza mechi 13 inakutana na Coastal Union ambayo ipo nafasi ya 12 na pointi 12.