>

YANGA WAREJEA DAR KAMILI KUIVAA MBEYA CITY

BAADA ya kumalizana na Dodoma Jiji kwa ushindi wa mabao 2-0 kikosi cha Yanga leo Novemba 23 kimerejea Dar kwa maandalizi ya mwisho dhidi ya Mbeya City.

Ni Novemba 26 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Mabao yote ya Yanga yalifungwa na mshambuliaji wao namba moja Fiston Mayele.

Kipindi cha kwanza alifunga bao moja na kipindi cha pili alifunga bao moja na kufanya afikishe mabao nane kibindoni.

Miongoni mwa wachezaji waliowasili Dar ni pamoja na Khalid Aucho, Dickson Ambundo, Mayele, Feisal Salum.