SIMBA MIKONONI MWA MBEYA CITY LEO SOKOINE

MBEYA City yenye maskani yake Mbeya ikiwa na staa Ssemujju Joseph ambaye ni mshambuliaji anayetumia nguvu nyingi na akili pamoja na winga mzawa Sixtus Sabilo, leo Novemba 23,2022 wataikaribisha Simba.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda kwenye mechi za nje ya mkoa wa Dar wamekuwa wakipata tabu kupata matokeo licha ya kuwa na wachezaji wenye uzoefu.

Ikumbukwe kwamba walishinda bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika dakika za lala salama kwa bao la Jonas Mkude walikwama kushinda mbele ya Singida Big Stars kwa sare ya kufungana bao 1-1 na hata mchezo wa kwanza kupoteza msimu huu ilikuwa ugenini.

Ni Azam FC iliwanyoosha bao 1-0 Simba Uwanja wa Mkapa hivyo leo wana kazi ya kujiuliza mbele ya Mbeya City.

Kwa upande wa ushambuliaji mastaa wawili wa timu hizo mbili ni wakali wa kucheka na nyavu ambapo Sabilo ni namba moja akiwa na mabao 7 huku Moses Phiri wa Simba yeye anayo mabao 6.

Hivyo kutakuwa na vita ya msako wa pointi tatu muhimu na msako wa kiatu cha ufungaji bora ambapo kwa sasa kiujumla kwenye ligi namba moja ni Fiston Mayele mwenye mabao 8.