SABABU ZA MUDA WA NYONGEZA KUWA KUBWA QATAR

TOKEA kuanza kwa michuano ya World Cup nchini Qatar Novemba 20,2022 kumekuwa na maswali mengi kwa wadau wa soka kutokana na ongezeko kubwa la muda wa ziada.

Hii imetokana na mabadiliko waliyofanya Fifa katika muda huo.

Sasa wanataka mpira uchezwe na dakika 90 zote zitumike.

Maana yake ule muda wa kutazama VAR, muda wa mchezaji aliumia lakini sasa hata ule muda wa kushangilia, wakati mpira umesimama inapigwa penalti vyote vinaingia kwenye muda wa ziada.

Hii ndio inafanya uone mpira sasa dakika za nyongeza ni 6,7 na wakati mwingine 10 hadi 11 na awali haikuwa hivyo.