>

SHABIKI WA SIMBA ASHINDA M 11 NA 10BET

SHABIKI wa Klabu ya Simba na Liverpool ya England Richard Mkumbo ameshinda Sh11 milioni kupitia jackpot ya katikati ya wiki ya kampuni ya 10 bet Tanzania.

Mkumbo ambaye ni mkazi wa Singida ameshinda kiasi hicho cha fedha baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 10 za ligi mbalimbali duniani kwa sh 500 tu.

 Ameweka kibindoni Sh11 milioni kati ya jackpot ya 10 bet Tanzania katikati ya wiki na kumfanya kuwa mshindi wa kwanza kuwahi kutokea Tanzania.

Mkumbo alitia kibindoni kiasi hicho baada ya kutabiri kwa usahihi mechi 10 za ligi mbalimbali duniani akiwa na Sh500 pekee.

Ushindi huo unamfanya Mkumbo kuwa mshindi wa kwanza wa jackpot hiyo hapa nchini na kukakabidhiwa zawadi yake na Meneja Masoko wa kampuni hiyo, George Abdulrahman katika hafla fupi ya makabidhiano.

Mkumbo amesema aliamua kubashiri na 10 bet kwa sababu kuwa na ‘odds’ iliyowekwa na kampuni hiyo katika mechi mbalimbali.

 “Mimi ni mjasiriamali na nimekuwa nikibashiri na 10 bet mara kadhaa na sikushinda. Hata hivyo sikukata tamaa na kuendelea na kufanikiwa kushinda milioni 11 kwa sh500 tu,” amesema Mkumbo.

Mshindi huyo aliwaomba vijana wenye umri kuanzia miaka 18 kubashiri na kampuni hiyo ili kushinda fedha kwa dau dogo tu.

“Ndoto yangu imetimia kwa sababu lengo la kubashiri na 10 bet ni kushinda na nimefanikiwa, nitaendelea kubashiri na kampuni hii,” amesema.

Amesema atazitumia fedha hizo kuendeleza biashara zake Dar es Salaam na Singida huku akisaidiana na ndugu zake katika masuala ya elimu.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa 10 bet Tanzania George Abdulrahman amesema wanajisikia fahari sana kubadilisha maisha ya Watanzania kupitia michezo yao ya kubashiri.

Kwa mujibu wa Abdurahman, Watanzania wengi wamekuwa wakitabiri na kujishindia fedha kupitia michezo yao ya kubashiri na kufanya mambo ya maendeleo.