MAYELE ABAINISHA KWAMBA HAWAJAHI ILI WAFUNGWE

FISTON Mayele, mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa hawajawahi kuelekea nchini Tunisia ili wafungwe bali watajitahidi kutafuta ushindi.

Kikosi cha Yanga kina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Club Africain kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa kesho Novemba 9,2022.

Tayari kikosi hicho kipo nchini Tunisia kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo ambao utaamua nani atasonga mbele kwenye hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho.

Mayele amesema:”Hatujawahi nchini Tunisia kwa ajili ya kuona tunapoteza mchezo wetu bali tunahitaji kupata matokeo mazuri na inawezekana mashabiki wawe pamoja nasi,” amesema.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 0-0 Club Africain.

Ikumbukwe kwamba Novemba 4,2022 kikosi cha Yanga kilisepa Dar kwa kupitia Dubai kisha kikaibuka nchini Tunisia kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo wa kimataifa.