AZIZ KI KIUNGO WA YANGA ‘OUT’

AZIZ KI nyota wa Yanga atakosekana kwenye mechi tatu zinazofuata kwa timu yake hiyo msimu wa 2022/23.

Sababu ya nyota huyo kukosekana kwenye mechi hizo ni maamuzi ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania ambayo yametolewa kutokana na kikao cha Novemba 4,2022.

Taarifa hiyo imetolewa leo Novemba 8,2022 ambapo kwa sasa Yanga ipo nchini Tunisia kwa ajili ya maandaizi ya mchezo wao dhidi ya Club Africain ya Tunisia.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa nyota huyo kwenye mchezo uliochezwa Oktoba 23,2022 alifanya kosa la kukwepa kusalimiana na wachezaji timu pinzani kabla ya kuanza kwa mchezo huo uliokamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Mbali na adhabu hiyo ya kukosa mechi tatu pia ametozwa faini ya laki tano.