>

WEKA KANDO KUSHINDWA KUSHINDA NYUMBANI,KIMATAIFA KAZI

 WEKA kando suala la kukosa matokeo kwenye mechi za kimataifa bado kwa wawakilishi wa kimataifa kwenye mechi za kimataifa kazi inaendelea kwa kuwa muhimu kupata matokeo.

Tunaona mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ilikuwa ngumu kwa wawakilishi wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Yanga kupata matokeo mazuri na sasa wana kazi nyingine ugenini.

Utani wa jadi umekuwa ukitawala hilo lipo wazi lakini ili kuendelea kutaniana kwa watani hawa ni lazima kila mmoja apate matokeo kwenye mechi ambazo anacheza na wakati ni sasa.

Unaona kwamba timu hazikubali kupoteza iwe ni nyumbani ama ugenini, hili ni jambo kubwa ambalo linastahili kuwa na mwendelezo.

Kila wakati ni muhimu kwa wachezaji kutambua kwamba mashabiki wanapenda furaha ambayo inapatikana kwenye matokeo mazuri.

Ukweli ni kwamba matokeo mazuri hayapatikani bila kuwa na maandalizi mazuri na kutekeleza yale ambayo yamepangwa kwenye uwanja wa mazoezi.

Iwe ni kwenye ligi hata mashindano ya kimataifa ni lazima kuwa na umakini hasa kwenye matumizi ya nafasi pamoja na kuwa wabunifu kwenye kila eneo ndani ya uwanja.

Kinachotakiwa kwa wawakilishi wetu kwenye mechi za kimataifa ni kila mmoja kucheza kwa umakini na kutumia vema nafasi ambazo wanazipata kwenye mechi na kuwapa furaha mashabiki.

Kila hatua ambayo inapigwa ni muhimu kufanya maandalizi mazuri kwenye mechi za kimataifa ambazo kinachohitajika ni ushindi kupata nafasi ya kusonga mbele hakuna jambo lingine.

Malengo ya wawakilishi wa Tanzania kimataifa ni kupata matokeo mazuri hivyo ni muhimu kila mmoja kulitambua hilo na kufanya kweli.

Inawezekana lakini kama hakutakuwa na mipango makini baada ya kumaliza mchezo mmoja kutakuwa na matokeo mengine tofauti na vile ambavyo mashabiki na uongozi wa timu husika unahitaji.

Kwa namna ambavyo timu itakuwa imeweza kufanya maandalizi yake itakuwa kwenye namna yake ya kupata matokeo.

Kwa kilichopatikana kwenye mechi zilizopita ni mpango kazi uliopangwa wakati uliopita kwa kazi iliyokuwa inafanywa kwenye uwanja wa mazoezi.

Kila timu ikiwa ugenini inakwenda na mbinu zake na ikiwa nyumbani pia inakwenda kwa mbinu zake hili ni la msingi kuzingatia na kuona kwamba kila kazi ina mpango wake maalumu.

Ipo wazi maisha ya kwenye mechi za kimataifa yana utofauti mkubwa na maisha ya ligi hasa kwenye upande wa mashindano husika na aina ya mechi ambazo zinachezwa kuwa na ushindani mkubwa.

Wachezaji kazi yao ni moja kufuata maelekezo ya benchi la ufundi ili kupata kile wanachokistahili,kikubwa ni mipango kazi na ushirikiano.

Ni wakati mzuri wa kujipanga tena na timu kuangalia yale ambayo waliweza kuyafanya msimu uliopita kitakachowapa nguvu kuendelea kwenye mechi zijazo ni kupata matokeo hakuna jambo lingine.

Kushiriki mashindano ya kimataifa ni fursa kwa wachezaji kuwa sokoni kwenye anga la kimataifa hili ni jambo kubwa ambalo litawafanya wazidi kuimarika na kuwa na thamani zaidi sokoni kitaifa na kimataifa.

Ipo wazi kwamba mashindano ya kimataifa yanahitaji maandalizi mazuri ili kuweza kupata matokeo chanya kwenye kila mechi.

Hakuna ambaye anapenda kuona kwamba kwenye mashindano ya kimataifa kwa mara nyingine tena kuona kila mmoja anashindwa kusonga mbele.

Wapinzani nao wanatambua kinachohitajika ni matokeo ya ushindi iwe mechi inachezwa ugenini ama nyumbani inawezekana kushinda.

Nina amini kwamba wachezaji ambao walishawahi kushiriki mashindano ya kimataifa wanaona  namna wanavyozidi kupata uzoefu kwenye kila hatua na hili ni jambo zuri.

Kadri ambavyo wanapata nafasi ya kucheza kimataifa wanaongeza hali ya uzoefu kwa wale wazawa inakuwa kazi nyingine ya kuongeza hali ya kujiamini pale watakapoitwa timu ya taifa ya Tanzania kutimiza majukumu mengine.

Jambo la muhimu ni maandalizi mazuri kwa mechi na kupata matokeo, wachezaji jitoeni bila kuogopa kwa ajili ya kupambania timu na kutimiza majukumu.

Muda ni sasa kuipeperusha bendera kimataifa na kuwapa furaha mashabiki ambapo furaha yenyewe inapatikana kwa kupata ushindi kwenye mechi zote uwanjani.