KOCHA Mkuu wa Simba, Juma Mgunda amesema kuwa wanatambua mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida Big Stars utakuwa na ushindani mkubwa.
Kikosi cha Simba leo Novemba 7 kimesepa Dar ambapo kitapitia Dodoma kabla ya kuibukia Singinda.
Mchezo huo wa ligi unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Liti ukiwa ni wa pili kwa Simba kucheza ugenini ule wa kwanza ilikuwa dhidi ya Tanzania Prisons.
“Tunatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu ambapo kila timu inahitaji matokeo lakini wapinzani wetu pia ni wagumu,” amesema Mgunda.