WAWAKILISHI wa Kanda ya Cecafa kwenye Mashindano ya Ligi ya Mabingwa Simba Queens, wametinga hatua ya nusu fainali baada ya kuvuna alama tatu mbele ya Green Buffaloes ya Zambia.
Ilikuwa ni mechi ya mwisho ya kundi A na ushindi wa mabao 2-0 umewapa uhakika wa kuungana na AS FAR Rabat kwenye hatua ya nusu fainali kwani kama wangefungwa wangekuwa wamefika mwisho.
Simba wamevuna jumla alama sita kwenye mechi tatu walizocheza huku Green Buffaloes wakiwa na pointi zao tatu kibindoni.
Pongezi kwa Simba Queens kwa kuipeperusha vema bendera ya Tanzania sasa hatua ya nusu fainali hii hapa kila la kheri.