>

KIBU MSHAMBULIAJI WA SIMBA MAMBO BADO KWAKE

BADO hajawa tegemeo ndani ya kikosi cha Simba msimu huu kwenye safu ya ushambuliaji ambapo kwenye mabao 17 yaliyofungwa na timu hiyo katoa pasi moja ilikuwa dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Sokoine alimpa mshikaji wake Jonas Mkude.

Mchezo huo ulikuwa ni wa kwanza wa Kocha Mkuu Juma Mgunda kuongeza kwenye ligi baada ya kupewa mikoba ya Zoran Maki.

Kibu Dennis bado anajitafuta kwa sasa akiwa kazi kubwa ya kufanya kwa msimu huu wa 2022/23 kuvunja rekodi yake ya msimu uliopita.

2021/22 alikuwa ni namba moja kwa watupiaji ndani ya kikosi cha Simba ambacho kiliyeyusha mataji yote kuanzia lile la ligi, Kombe la Shirikisho na Ngao ya Jamii ambayo yalikwenda Yanga.

Alitupia jumla ya mabao 8 baada ya kucheza mechi 21 na alitoa jumla ya pasi nne za mabao.

Mgunda amesema kuwa wachezaji wote wana kazi ya kutafuta ushindi kwa ajili ya timu jambo ambalo wanalifanya kwa ushirikiano.

“Ikitokea akaanza ama akawa benchi bado ni mchezaji wa Simba kwani kinachotakiwa ni kuona anafanya vizuri na amesajiliwa kwa ajili ya kucheza.

“Matokeo ni kitu ambacho kinahitajika bila kujali nani amefanya nini na amepewa muda upi. Makosa ambayo yanatokea tunayafanyia kazi ili kuwa imara wakati ujao,” .