>

NABI: WACHEZAJI WOTE WAPO TAYARI KIMATAIFA

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wachezaji wote wapo tayari kwa mchezo wa kesho wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Club Africain.

Ni Uwanja wa Mkapa ukiwa ni mchezo wa mtoano wa kwanza na ule wa pili tachezwa nchini Tunisia.

Kocha amesema:”Wachezaji wako tayari na wameahidi kupambana, tunaomba sapoti kwa mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi, nguvu yao ni muhimu sana kwenye mchezo wetu wa kesho.

“Kila mmoja anataka kuona tunapata matokeo hilo lipo wazi nasi tunahitaji kufanya vizuri kikubwa ni kila mmoja kucheza kwa kujiamini na kufuata maelekezo kwani mchezo wa mpira ni tofauti na michezo mingine.

“Club Africain wana timu nzuri na Wachezaji wenye uzoefu pamoja na Wachezaji chipukizi. Ni wazuri kwenye mipira ya kufa na mashambulizi ya haraka, pamoja na kwamba tunahitaji matokeo mazuri nyumbani pia tutacheza kwa tahadhari tusiruhusu goli”