>

DUBE APELEKA MAUMIVU IHEFU

 MGUU uleule uliowapa tabu Simba, Uwanja wa Mkapa ndani ya 18 umegeuza kibao kwa mara nyingine mbele ya Ihefu.

Mtupiaji yuleyule aliyempa tabu Air Manula sasa tabu iligeukia upande wa Ihefu kwa kipa Fikirini.

Kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara jana dhidi ya Ihefu, nyota Dube alifunga bao kwa mguu wake wa kulia likiwa ni bao la ushindi kwa Azam FC na kupeleka maumivu kwa mashabiki na wachezaji wa Ihefu.

Ni dakika ya 55 Dube alipachika bao hilo Uwanja wa Azam Complex na kuipa pointi tatu muhimu Azam FC.

Azam FC inafikisha pointi 17 ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi huku Ihefu ikibaki na pointi tano nafasi ya 14.