>

YANGA YASEPA NA POINTI TATU KWA PENALTI ILIYOZUA GUMZO

DAKIKA 45 za jasho zimekamilika Uwanja wa CCM Kirumba ambapo ubao umesoma Geita Gold 0-1 Yanga.

Kwenye kikosi cha Yanga kiungo Feisal Salum alianza na alikuwa akipambana kwa nguvu kubwa na nyota wa zamani wa timu hiyo Adeyum Saleh.

Bao pekee la ushindi limefungwa na kiungo Bernard Morrison kwa pigo la penalti dakika ya 45.

Penalti hiyo imezua gumzo kwa wachezaji kutokana na mazingira yake ilivyopatikana na mwamuzi wa kati kuamua lipigwe tuta.

Jitihada za Geita Gold kupata bao wakiwa na kiungo wao Said Ntibanzokiza ziligonga mwamba na kuwafanya wapoteze pointi tatu mazima.

Yanga inafikisha mechi 45 za Ligi Kuu Bara bila kupoteza tangu msimu wa 2021/22.