>

MIPANGO YA SIMBA KUMTUMIA MZAMIRU ILIKWAMA HIVI

MZAMIRU Yassin kiungo wa kazi ndani ya Simba mchezo wake wa kwanza kutokuwa kwenye mpango wa benchi la ufundi msimu wa 2022/23 ilikuwa dhidi ya Azam FC kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Hakuwa kwenye mpango wakati timu hiyo ikinyooshwa kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Mkapa Oktoba 27,2022.

Nyota huyo mzawa ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Juma Mgunda kutokana na uimara wake akiwa eneo la kati kwenye kuzima mashambulizi na kucheza kwa utulivu.

Kadi yake ya kwanza ya njano msimu wa 2022/23 kwenye ligi aliipata kwenye mchezo dhidi ya  Tanzania Prisons, Uwanja wa Sokoine wakati akiyeyusha dakika 90 na ubao ulisoma Prisons 0-1 Simba, alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 90.

Mchezo wa pili kuonyeshwa kadi ya njano ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji wakati ubao ukisoma Simba 3-0 Dodoma Jiji, alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 86.

Kete ya mwisho iliyokamilisha idadi ya kadi tatu za njano ilikuwa kwenye mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Yanga ubao uliposoma Yanga 1-1 Simba, alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 26 baada ya kumchezea faulo kiungo Jesus Moloko.

Jumla kacheza mechi 6 za ligi akiwa ameyeyusha jumla ya dakika 346 msimu wa 2022/23.