>

FEISAL KUONGEZA ZAIDI JUHUDI YANGA

 KIUNGO wa Yanga, Feisal Salum amesema kuwa atazidi kuongeza juhudi katika kutengeneza nafasi na kufunga pale anapopewa nafasi ya kucheza.

Kiungo huyo mzawa ni namba moja kwa mastaa wenye mabao mengi ndani ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Bao lake la nne alipachika kwenye mchezo wa ligi dhidi ya KMC uliochezwa Uwanja wa Mkapa ambapo alifunga akitokea benchi.

Yanga ni namba moja kwenye msimamo ikiwa na pointi 17 huku nafasi ya pili ikiwa mikononi mwa Mtiwa Sugar yenye pointi 15.

Fei amesema:”Ninaahidi kuendelea kufunga na kutengeneza nafasi kwa ajili ya timu yangu na wachezaji ili kupata ushindi kwenye mechi ambazo tunacheza.

“Kikubwa ni kuona kwamba kila kitu kinaendelea kuwa vizuri na rekodi yetu ya kutofungwa inaendelea kwani ushindi ni jambo la msingi,” .