INAELEZWA kuwa Nasreddine Nabi amefikia makubaliano ya kuachana na Yanga kutokana na kushindwa kufikia malengo ambayo yalipangwa.
Timu hiyo malengo makubwa ilikuwa ni kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika iligotea kwenye hatua za mtoano kwa kuodolewa kwa jumla ya mabao 2-1 dhidi ya Al Hilal.
Mchezo wao wa ligi dhidi ya Simba ilikuwa ni kipimo kingine kwake na badala yake alipata pointi moja kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Habari zinaeleza kuwa sababu ya Nabi kutimka ndani ya Yanga ni kutokuwa na maelewano mazuri na msaidizi wake Cedric Kaze.
Hivi karibuni, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe alibainisha kuwa hawana mpango wa kumfuta kazi Nabi.
“Yote hayo yanayosemwa hakuna ukweli, Nabi bado ni kocha wa Yanga na ana endelea na majukumu yake ndani ya timu,”.
Mchezo ujao wa Yanga kwenye ligi ni dhidi ya KMC unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Oktoba 26.