WAAMUZI wa mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga v Simba wametangazwa.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Oktoba 23, Uwanja wa Mkapa ambapo kiingilio kwa mzunguko ni 5,000.
Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, (TPLB) imemtaja Ramadhan Kayoko kuwa ni mwamuzi wa kati.
Pia wengine ambao atafanya nao kazi kwenye mchezo huo ni pamoja na Mohamed Mkono assistance 1, Janeth Balama assistance 2, Elly Sassi 4th huku kamishna wa mchezo akiwa ni Kamwanga Tambwe.