MFANYABIASHARA ya Mbao, anayetokea Mufindi wilaya ya Mafinga, Iringa
Maliki Athumani Mshuza, ameshinda sh. 15,626,306 katika Jackpot Bonus ya Sportpesa iliyochezwa katikati ya wiki iliyoisha, baada ya
kupatia kwa usahihi mechi 12 kati ya mechi 13.
Akizungumza baada ya hafla ya makabidhiano ya mfano wa hundi katika ofisi za Sportpesa jijini Dar, Maliki amesema alianza
kucheza na Sportpesa katikati ya mwaka 2021, akiwa hakumbuki mwezi kamili.
‘’Nilianza kucheza na Sportpesa mwaka mmoja uliopita. Unajua pale ninapoishi kuna watu wengi wanacheza michezo ya kubashiri, hivyo
walinishawishi lakini nilichukua muda kidogo kukubaliana nao kama na mimi nianze kubashiri kama wao.
Kwa mujibu wa maelezo yake, Maliki anasema kila jioni mara nyingi alikuwa anawaona vijana wenzie mmoja mmoja ama kwa vikundi
wakikaa pamoja wanaonyeshana simu na mara nyingine wanafurahi pamoja au wanasononeka kwa pamoja.
Lakini mara nyingi alikuwa akiwaona wakifurahia hivyo na yeye kwa
sababu alikuwa karibu yao wakawa wanamshawishi kwa nini na yeye
asiweke bashiri zake kama wao.
Akielezea namna alivyopata ushindi huu wa Jackpot bonus ya katikati
ya wiki, Maliki anasema yeye ana mazoea ya kuweka mkeka mmoja tu na si zaidi ya hapo.
“Mimi sichezi Multibet au single bet. Mimi nacheza hizi Jackpot tu. Mazoea yangu kila mkeka ukitoka mara nyingi huwa
najipa siku tatu nachambua timu taratibu usiku kabla ya kulala nikiwa
nimetullia.
Maliki anasema kuwa akishaweka mkeka huwa hafuatilii mikeka yake kwa kuitazama kwenye TV au kwa kutumia app za matokeo kwa sababu hataki presha.
“Mimi nikishaweka mkeka huwa nauacha mpaka mechi ziishe ndipo nakuja kuangalia matokeo. Sasa kwa mkeka huu ulioshinda nilikuwa nyumbani nimetulia na simu
nimeiacha mbali kidogo ina chaji, baadae nilipigiwa simu na washkaji
zangu kwamba tukaonane. Wakati najiandaa kutoka iliingia sms ikinipa hongera kwa kushinda. Nilipoitazama vizuri ndio ulikuwa ushindi huu.
Maliki anawashauri watanzania wacheze kwa wingi SportPesa hasahasa Jackpot kwani hata kama hujashinda Jackpot yenyewe una nafasi
ya kupata bonus kama yeye alivyopata.
“Mimi nilichukua muda kukubaliana na uhalisia huu. Ukiachia shughuli yangu ya biashara ya
mbao, huku kwenye kubashiri ni kama kitu cha ziada mabacho hakikugharimu muda mwingi wala pesa nyingi. Unaweka buku tu na
kusubiria matokeo’’.
Naye Meneja Uhusiano na Mawsasiliano wa Sportpesa, Sabrina Msuya alimpongeza Maliki kwa ushindi na kumtaka aendelee kupambania
ndoto zake za kuibuka na Jackpot za SportPesa bila kuchoka.
Hivi sasa Jackpot kubwa ya SportPesa imefikia sh. 1,042,926,769.
“Kipekee nikupongeze kwa uamuzi wako wa kucheza Jackpot. Kama ambavyo leo umetoa ushuhuda umeanza kucheza rasmi mwaka jana na sasa umevuna matunda kwenye Jackpot bonus, basi nikutakie kila la kheri kwenye ndoto zako’’ alimalizia Sabrina.