BUKU TANO TU KUWAONA AZIZ KI, PHIRI NA MAYELE

KUELEKEA mchezo wa Ligi Kuu Bara wa Kariakoo Dabi kati ya Yanga v Simba buku tano tu inatosha kuona dakika 90 za jasho.

oKTOBA 23,2022 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwa kila timu kupambania pointi tatu.

Yanga ambao ni wenyeji wa mchezo huu tayari wamebainisha viingilio kwa ajili ya mashabiki kuona burudani itakayotolewa na mastaa wao ikiwa ni pamoja na Feisal Salum, Aziz KI, Fiston Mayele na Khalid Aucho.

Kwa upande wa Simba wao mastaa wao ni pamoja na Moses Phiri, Sadio Kanoute, Habib Kyombo na Kibu Dennis.

Bei za viingilio zipo namna hii:-

VIP A ni 30,000

VIP B ni 20,000

VIP C ni 15,000

Machungwa ni 10,000

Mzunguko ni 5,000 Uwanja wa Mkapa saa 11:00 jioni