MCHEZO WA KMC V AZAM WABADILISHWA TAREHE, IBWE APATA SHAVU

MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya KMC v Azam FC umebadilishwa tarehe kutoka ile ya awali ambayo ilipangwa.

Oktoba 22 mchezo huo wa ligi ulitarajiwa kuchezwa na sasa utapigwa Oktoba 21.

Taarifa iliyotolewa na idara ya habari KMC imeeleza kuwa sababu ya mabadiliko hayo ni kupisha mchezo wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 23 kucheza mchezo wa kuwania kufuzu AFCON.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Otoba 22 kati ya Tanzania na Nigeria.

Azam FC ambao leo wamemtangaza Ofisa Habari wa muda Hasheem Ibwe akichukua mikoba ya Zakaria Thabit ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa miezi mitatu imetoka kucheza mchezo wa kimataifa dhidi ya Al Akhdar na kuondolewa kwenye Kombe la Shirikisho kwa jumla ya mabao 3-2.

KMC imetoka kushinda mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo wao uliopita wa ligi.