>

KIMATAIFA YANGA MIKONONI MWA WAARABU

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho, Yanga wamepangwa kucheza na Club Africain kutoka Tunisia.

Ni kwenye michezo ya mtoano kutafuta timu zitakazoingia hatua ya makundi ya michuano hiyo ambayo ni ya pili kwa ukubwa  kwa ile inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika, (Caf)

Mechi ya kwanza mtoanoinatarajiwa kuchezwa Novemba 02, Uwanja wa  Benjamin Mkapa na marudiano kuwa Novemba 09.

Yanga imeangukia hapo baada ya kutolewa kwa jumla ya mabao 2-1 dhidi ya Al Hilal uliochezwa Sudan.

Kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Yanga iliambulia sare ya kufungana bao 1-1 na ule wa pili ikiwa ugenini ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.