IMEWACHUKUA dakika 33 wachezaji wa Simba kusaka bao la kuongoza kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya de Agosto.
Ni bao la Moses Phiri dakika ya 33 limefungua ukurasa wa uongozi kwa wenyeji Simba.
Amepachika bao hilo akiwa kwenye uangalizi wa mabeki wa de Agosto akitumia pasi ya nahodha msaidizi Mohamed Hussein.
Kwa sasa ni mapumziko, Simba inakwenda vyumbani ikiwa na mtaji wa mabao 4-1.