>

HUYU HAPA AMETAJWA KUIPELEKEA SIMBA HATUA YA MAKUNDI

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa Kocha Mkuu Juma Mgunda wana imani naye atawapeleka hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kupata ushindi dhidi ya de Agosto ya Angola.

Leo Simba inakibarua cha kusaka ushindi Uwanja wa Mkapa ikiwa na mtaji wa mabao 3-1 iliyopita ugenini dhidi ya de Agosto inahitaji kulinda ushindi huo ili kusonga mbele.

Ahmed Ally, Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa hawana hofu na wapinzani wao kutokana na uwezo wa wachezaji.

“Kocha Juma Mgunda ni kocha wa mpira tunaamini kuwa tunakwenda kucheza hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika na inatokana na ubora wa wachezaji ambao tupo nao ikiwa ni pamoja na Clatous Chama, Moses Phiri wote wapo vizuri.

“Uwanja wa Mkapa sio sehemu salama kwa wapinzani na wao wanajua hilo makosa ambayo tulifanya wakati uliopita hatutarudia tunahitaji ushindi.

“Kwa namna ambavyo wachezaji wanajua kuhusu uzuri wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya Makundi watafanya kazi kubwa, itakuwa ni siku ya burudani wakati timu inatinga hatua hiyo kubwa Afrika.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia burudani kila kitu kinakwenda sawa ndio maana hamasa inafanyika kwa wakati ili wafike kwa wingi uwanjani,” amesema Ally.

Mgunda anafanya kazi kwa ukaribu na Seleman Matola ambaye ni msaidizi wake na wote ni wazawa.