KMC HESABU ZAO NI KUELEKEA MTIBWA SUGAR

 BAADA ya ubao wa Uwanja wa Uhuru kusoma KMC 0-0 Ruvu Shooting, Oktoba 7,2022 hesabu za wazee wa pira kodi ni kuelekea mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala ameweka wazi kuwa maandalizi yanakwenda sawa na wachezaji wana morali kubwa kuelekea mchezo huo.

Christina amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo ambao wanahitaji pointi tatu.

“Mchezo ujao dhidi ya Mtibwa Sugar kwa sasa wachezaji wanaendelea kujiandaa na mchezo wetu ambao ni muhimu na tunahitaji pointi tatu.

“Uzuri ni kwamba mwalimu anawajua wachezaji wake mapungufu yaliyopita na sasa kuelekea mchezo ujao tunaamini tutapata pointi tatu,” amesema Christina.