KAZI IMEANZA KWA SIMBA KUWAKABILI WAANGOLA

AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema mashabiki watakaojitokeza Uwanja wa Mkapa watakutana na bendera za rangi nyekundu na nyeupe ili kuongeza nguvu kwenye kushangilia kwa kuzipunga juu kama walivyofanya Simba Day.

Aidha ameongeza kuwa kuelekea mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya de Agosto, Oktoba 16,2022 Uwanja wa Mkapa wapo tayari na wachezaji wameanza mazoezi.

“Kikosi chetu kimerejea rasmi mazoezini baada ya juzi kurejea kutokea Angola. Jana asubuhi wachezaji walianza mazoezi kwenye uwanja wa Mo Simba Arena na leo wataendelea na mazoezi jioni.

“Tulishinda lakini bado hatujafuzu, safari hii hatutaki kurudia makosa. Tumeweka nguvu kubwa kuona kwamba mchezo wa jumapili tunapata matokeo mazuri ili tuingie makundi. Tumemiss kushiriki hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.”

Walipocheza ugenini, Simba ilishinda mabao 3-1 hivyo wanakwenda kurejeana wakiwa wanaongoza katika dakika 90 za mwanzo.