MRITHI WA MIKOBA YA DJUMA HUYU HAPA

MELIS Medo, ametangazwa kuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Dodoma Jiji kwa msimu wa 2022/23.

Kocha huyo anachukua mikoba ya Masoud Djuma ambaye alifikia makubaliano ya kuachana na timu hiyo Oktoba 10,2022.

Sababu kubwa ya Djuma ambaye aliwahi kuwa kocha msaidizi ndani ya Simba ni kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo msimu wa 2022/23 kwenye mechi za mwanzo.

Mchezo wa mwisho Djuma alishuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 3-0 Dodoma Jiji.

Medo aliwahi kuwa kocha wa Coastal Union pamoja na Insta United sasa anakuwa kwa wakulima wa Zabibu.

Mchezo ujao wa Dodoma Jiji ni dhidi ya Ihefu unatarajiwa kuchezwa Oktoba 16 itakuwa ni kete yake ya kwanza kukaa benchi.