HIZI HAPA DAKIKA ZA PHIRI NA MABAO YAKE KWENYE LIGI

MZEE wa saluti hana ushikaji na makipa ndani ya Ligi Kuu Bara pale anapopata nafasi kwa kuwa amekuwa akiwadhibu namnaanavyotaka iwe nje ya 18 ama ndani ya 18.

Ni Moses Phiri raia wa Zambia ambaye ni namba moja kwa utupiaji kwenye kikosi hicho akiwa ametupia mabao manne, tupo naye kwenye mwendo wa data namna hii:-

Mechi za Ligi-5

Dakika zake ni 395

Mabao 4

Eneo

Nje ya 18 bao 1

Ndani ya 18 mabao matatu

Viungo

Amefungwa kwa kichwa bao moja

Amefunga kwa mguu wa kushoto mabao mawili

Amefunga kwa mguu wa kulia bao moja

Dakika zake

Dakika 61 mbele ya Geita Gold

Dakika 66 mbele ya Kagera Sugar

Dakika 90 mbele ya KMC

Dakika 90 mbele ya Tanzania Prisons

Dakika 88 mbele ya Dodoma Jiji

Timu alizozifunga ni 4

Geita Gold

Kagera Sugar

KMC

Dodoma Jiji