JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa ushindi ambao wameupata ugenini kwenye mchezo dhidi ya de Agosto ya Angola unatokana na jitihada za wachezaji pamoja na mipango ya Mungu.
Kikosi cha Simba jana Oktoba 9,2022 kiliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya de Agosto kwenye mchezo ambao walikuwa ugenini.
Leo kikosi kimerejea kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudio unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, wikiendi hii na ni dege lakukodi wametumia.
Mabao ya Clatous Chama, Moses Phiri na Israel Mwenda yameipa uongozi Simba ikiwa inakibarua cha kulinda ushindi wao ili waweze kutinga hatua ya makundi.
Mgunda amesema:”Tumepata ushindi tukiwa ugenini tunamshukuru Mungu, wachezaji wamejituma kwenye kutimiza majukumu yao na kazi bado ipo kwa kuwa kuna mechi nyingine inakuja.
“Kwa sasa akili zetu ni mchezo wetu wa marudio ambao tunaamini kwamba utakuwa na ushindani mkubwa, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kazi bado haijaisha,” .