MZAWA Feisal Salum mali ya Yanga amefikisha jumla ya mabao matatu ndani ya kikosi hicho akiwa sawa na Fiston Mayele raia wa DR Congo.
Bao la tatu Fei Tofo amefunga leo Oktoba 3,2022 kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Mkapa.
Baada ya dakika 90 uao umesoma Ruvu Shooting 1-2 Yanga ambapo bao la ufunguzi lilikuwa la Fei dakika ya 52 kwa pigo la kichwa na lile la pili limefungwa na nahodha Bakari Mwamnyeto dakika ya 71.
Ruvu Shooting wamepachika bao la kufutia machozi kupitia kwa Rolland Msojo dakika ya 85