MSHAMBULIAJI wa Simba, Moses Phiri ametangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora waMashabiki ndani ya mwezi Septemba.
Ni mashabiki ambao walikuwa wanachagua kwa kupiga kura kupitia mitandao ya kijamii ambapo ni Phiri alikuwa ameingia fainali na Mzamiru Yassin pamoja na Clatous Chama kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).
Taarifa iliyotolewa na Simba imeeleza kuwa tuzo hiyo kwa mwezi Septemba inakwenda kwa Phiri.
Ikumbukwe kwamba mwezi Agosti ilikwenda kwa Chama ambaye aliwashinda Sadio Kanoute na Pape Sakho.