BONDIA Mtanzania Ibra class amefanikiwa kumchapa bondia Alan Pina anayetoka Mexico kwenye Pambano la raundi 12.
Pambano hilo lilikuwa na vuta nikuvute nyingi lakini halikuwa la ubingwa lililofanyika Mlimani City jijini Dar es salaam.
Tangu Mwanzo wa pambano hilo Pina alionyesha upinzani mkali kwa Ibrahimu Class mpaka ilipofika raundi ya 9 na kumfanya Mtanzania huyo ashinde kwa K.O
Alan Pina alipigwa ngumi mbili nzito ambazo zilimpelekea kwenda chini na kudaiwa kupoteza fahamu na hivyo kulazimika kupewa huduma ya haraka ili kunusuru maisha yake.
Aidha, kutokana na ushindi huo Tanzania inaendelea kuandika rekodi mpya katika mchezo wa ndondi baada ya mabondia wake wengi kuendelea kufanya vizuri katika mapambano mbalimbali ya ndani pamoja na yale ya kimataifa.