MAYELE, FEISAL WAFANYA YAO YANGA IKISHINDA

FISTON Mayele mzee wa kutetema ni miongoni mwa nyota ambao walicheka na nyavu kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Mbuni FC ya Arusha uliochezwa Uwanja wa Avic Town.

Mayele ni mshamuliaji namba moja ndani ya Yanga kutokana na kasi yake kuendelea pale ambapo aliishia msimu uliopita.

Kwenye ligi Mayele katupia mabao matatu baada ya kucheza mechi nne huku kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya kwanza katupia mabao sita.

Alitupia mechi mbili mabao matatumatatu kila mechi na kumfanya asepe na mipira miwili kwenye mechi hizo na hatua inayofuata wanacheza na Al Hilal.

Yanga ilishinda mabao 2-1 ambapo ni mabao ya Mayele na Feisal Salum waliweza kufunga kwenye mchezo huo.

Ni bao la Jesto Masanja hili lilifungwa kwa upande wa mbinu FC kipindi cha pili cha mchezo huo..

Mbuni inayoshiriki Championship malengo yao makubwa ni kupanda Ligi Kuu Bara msimu ujao.