LIGI INAREJEA WACHEZAJI MUHIMU KUWA NA NIDHAMU

 REKODI kwa wachezaji wale ambao wanafungiwa mechi zao kutokana na kuonyesha nidhamu mbaya katika Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2022/23 haipaswi kupewa nafasi.

Wakati mwingine kwa sasa ni mwendelezo wa ligi baada ya muda wa mapumziko kutokana na mechi ambazo zilikuwa zinaendelea kwenye timu za taifa.

Ukweli ni kwamba kurejea kwa ligi ni muhimu kila mmoja kuongeza umakini kwenye ushindani wa ligi ambao unaendelea kwa msimu huu.

Nidhamu ipewe kipaumbele kwenye kila mchezo ambao  utachezwa bila kujali nani ambaye anaanza kwenye mchezo wa kwanza.

Benchi la ufundi pamoja na wachezaji kuna makossa ambayo waliyaona kwenye mechi zilizopita jambo lililowafanya wakakosa matokeo.

Kwa zile ambazo zilizopata matokeo ni muhimu kuwa kwenye mwendelezo mzuri ili kupata kile ambacho wanakipata.

Ugumu upo na kila timu inahitaji kupata matokeo chanya kwa kuwa ligi inarudi basi muhimu kila mmoja kupambania malengo yake.

Hakuna namna ligi inarudi basi burudani irejee makosa ya wachezaji yasijirudie na waamuzi waongeze umakini kwenye mechi zote wanazocheza.

Tunaamini kwamba burudani itakuwa nzuri na ushindani utakuwa imara kwa kila mmoja ambaye atapata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza.

Kwa maandalizi ya timu za taifa kwenye kambi zilizowekwa ni muhimu kila mchezaji kufanya maandalizi mazuri.

Kila kitu kinawezekana kwa kuzingatia maandalizi mazuri na muhimu kupata matokeo kwenye mechi wanazocheza.

Ruvu Shooting leo watakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya Coastal Union, Uwanja wa Uhuru.

Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkuwa kwa kuwa kila timu inahitaji pointi tatu hivyo muhimu ni kufanya maandalizi muhimu na kucheza kwa nidhamu.

Pia kwa timu ambayo haijapata pointi kwenye ligi ambayo ni Ihefu ni muhimu kufanyia kazi makosa yao.