HAJI MANARA AMPA PONGEZI ALLY KAMWE KUTEULIWA YANGA

ALLY Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa baada ya kutangazwa rasmi kwenye Idara ya Habari na Mawasiliano alipongezwa na Haji Manara ambaye ni Msemaji wa Yanga.

Ameweka wazi kuwa Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba naye alimpa pongezi.

Septemba 27, Kamwe alitangazwa kuwa Ofisa Habari na Priva Abiud maarufu kama Privaldinho alitangazwa kuwa Msimamizi Mkuu wa Digital na Maudhui.

Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na +255 Global Radio kwenye kipindi cha Krosi Dongo, jana Kamwe alisema kuwa alijisikia kuwa mwenye furaha baada ya kutangazwa kuanza majukumu mapya.

“Baada ya kutangazwa nimepewa pongezi nyingi ikiwa ni pamoja na kutoka kwa Haji Manara na Ahmed Ally, Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano ndani ya Simba wote wamefurahi mimi kutangazwa.

“Nilifurahi nilipopewa taarifa hizi kwa kuwa mimi ni shabiki wa Yanga na kazi kubwa ambayo nitafanya ni kushirikiana na wengine ili kufikia malengo yetu,” alisema Kamwe.