KWENYE mchezo wa kirafiki dhidi ya Malindi uliochezwa Uwanja wa Amaan kipa namba tatu wa Simba, Ally Salim aliweza kuonyesha uwezo wake kwa kuanza kikosi cha kwanza.
Leo Septemba 28,2022 kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda kina kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo mwingine dhidi ya Kipanga FC ndani ya dakika 90.
Mgunda ameweka wazi kuwa maandalizi yapo sawa na wanaimani ya kupata ushindi kwenye mchezo huo ambao utakuwa na ushindani.
“Wachezaji watakuwa na kazi kubwa ya kusaka ushindi, kila mmoja atafanya kazi kubwa na hilo litatupa matokeo mazuri.
“Ushindi wa mchezo uliopita ni moja ya kazi ambayo inatufanya tuamini kwamba kazi bado ipo na wachezaji wanazidi kuwa imara,” amesema.
Kwenye mchezo wa kwanza wa kirafiki Simba ilipata ushindi wa bao 1-0 walipata dhidi ya Malindi bao ambalo lilifungwa na Nassoro Kapama kwa pasi ya Peter Banda aliyepiga kona dakika ya 13.