PETER Banda na Nassoro Kapama wameibuliwa na Malindi FC kwenye mchezo wao wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Kwenye mchezo huo uliochezwa juzi, ubao ulisoma Malindi0-1 Simba huku bao la ushindi likifungwa na Nassoro Kapama dakika ya 13.
Bao hilo ni la kwanza kwa Kapama ambaye ameibuka ndani ya Simba akitokea Kagera Sugar na inakuwa pasi ya kwanza kwa Banda msimu huu wa 2022/23 akiwa na uzi wa Simba.
Kesho kikosi cha Simba kinachonolewa na Juma Mgunda kinatarajiwa kucheza mchezo wa pili wa kirafiki dhidi ya Kipanga.
Mgunda amesema kuwa maandalizi yapo sawa na wanaamini mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa.
“Tupo tayari kwa ushindani na kila kitu kinakwenda sawa tunaamini kwamba ushindani utakuwa mkubwa na kila kitu kitakuwa sawa,”.