MGUNDA; TUPO TAYARI KUIKABILI MALINDA

 JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya Malindi, Uwanja wa Amaan.

Simba imealikwa kwenye mashindano maalumu Visiwani Zanzibar na leo itacheza mchezo wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Malindi.

Jana Septemba 24 kikosi hicho kilifanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa leo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Mgunda amesema;”Kila kitu kinakwenda sawa na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu na tunaamini kwamba tutapata matokeo mazuri.

“Mpangilio mzima na namna ambavyo wachezaji wanafurahia mazoezini inaonesha kuna kitu kipo hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,” amesema Mgunda.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo Zanzibar ni pamoja na Pape Sakho, Sadio Kanoute, Erasto Nyoni, Mohamed Hussein, Joash Onyango.