KOCHA MOSIMANE APATA DILI SAUDI ARABIA

KLABU ya Soka ya Al-Ahli kutoka Saudi Arabia leo Jumapili Septemba 25, 2022 imemtangaza Pitso Mosimane kuwa Kocha Mkuu wa Klabu hiyo.

Kabla ya Mosimane kujiunga na klabu hiyo alikuwa akiitumikia Klabu ya Al Ahly ya Misri.

Al-Ahli inashiriki Ligi Daraja la pili nchini Saudi Arabia baada ya kushuka daraja msimu uliopita wa 2021/ 2022.

Mpango wa kujiunga na Simba sasa umekwama jumlajumla kwa kuwa ameshapata changamoto mpya.

Jina la kocha huyo lilikuwa linatajwa kuwa miongoni mwa wale ambao wanaweza kufanya kazi Simba.