TIMU YA TAIFA U 23 YAWAFUATA SUDAN KUSINI

KIKOSI cha Timu ya Taifa ya Vijana Chini ya Miaka 23, leo Septemba 24 kimeanza safari kuelekea Rwanda.

Kinatarajiwa kucheza na Timu ya Taifa ya Sudan Kusini kwenye mchezo wa marudiano kuwania kufuzu AFCON.

Mchezo wa kwanza uliochezwa jana Septemba 23, Uwanja wa Azam Complex ubao ulisoma Tanzania 0-0 Sudan Kusini.

Hemed Morocco, Kocha Mkuu wa U 23 amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na makosa watayafanyia kazi.

“Kikubwa ambacho tulikuwa tunahitaji mchezo wetu wa kwanza ni matokeo, kushindwa kuyapata imetokana na kushindwa kutumia nafasi ambazo tumezipata hivyo tunakwenda kufanya vizuri mchezo wetu ujao.

“Mchezo wetu umepita na tumeshindwa kupata matokeo hivyo tutakwenda kupambana kupata matokeo mchezo ujao,” amesema.

Miongoni mwa mastaa ambao wameondoka na kikosi hicho ni pamoja na nahodha Kelvin John, Tepsi Evance, Davi Kameta na Aboutwalib Mshery.