TAIFA STARS KUSUKWA UPYA KIMATAIFA

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars,Honour Janza, amesema kuwa mechi za kirafiki za kimataifa zilzio kwenye Kalenda ya FIFA zitampa mwanga wa kusuka kikosi imara kwa ajili ya ushindani.

 Stars inatarajiwa kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Uganda na Libya na zitachezwa nchini Libya na tayari kikosi hicho kimeshatua nchini humo baada ya kuondoka Bongo Septemba 20.

 Kocha huyo amesema: “Mechi mbili tunatarajia kucheza hizi ni faida kwetu hasa kwenye kuunda kikosi kipya na kuangalia namna kile ambacho tunawafundisha wachezaji wanaonyesha kwa vitendo.

“Nimeona vipaji vingi vipo kwa wachezaji wale wenye uzoefu mkubwa na wale ambao ni chipukizi, kikubwa ni kila mmoja kupata nafasi na kuitumia kwa umakini,”.

Tanzania itaanza kucheza na timu ya Taifa ya Uganda Septemba 24 na mchezo wa pili dhidi ya Libya unatarajiwa kuchezwa Septemba 27.