KIMATAIFA:YANGA 0-0 ZALAN FC

UWANJA wa Mkapa, mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya awali ubao unasoma Yanga 0-0 Zalan, FC.

Hakuna mbabe kwa timu zote mbili kwa sasa ndani ya dakika 45 huku Yanga ikionekana kuanza kwa kasi kuliandama lango la Zalan FC.

Mashuti 8 Yanga wamepiga hajalenga lango huku Zalan FC wao wakipiga shuti moja ambalo limelenga lango.

Yanga ina faida ya mabao 4-0 ambayo ilishinda kwenye mchezo wa awali uliochezwa Uwanja wa Mkapa huku wenyeji wakiwa ni Zalan na Fiston Mayele alitupia mabao matatu huku mzawa Feisal akitupia bao moja.