MKALI WA MIPIRA MIREFU AMEFUNGUA AKAUNTI YA MABAO

HASSAN Nassoro kiungo wa Mbeya City ni miongoni mwa wazawa wenye uwezo wa kupiga mipira mirefu ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kiungo huyo mwenye rasta kichwani ni ingizo jipya ndani ya Mbeya City akitokea kikosi cha Dodoma Jiji.

Alikuwa miongoni mwa nyota walioshuhudia timu hiyo ikipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Singida Big Stars mchezo uliochezwa Uwanja wa Liti.

Singida Big Stars yenye mastaa kadhaa ikiwa ni pamoja na Juma Abdul, Amis Tambwe, Meddie Kagere ina mtaalamu mmoja wa kupiga mipira mirefu.

Ni beki wa kati ambaye ni nahodha pia, Pascal Wawa huyu naye ni ingizo jipya ndani ya Singida aliibuka hapo akitokea Simba.

Nassoro ana bao moja kibindoni ambalo alifunga Uwanja wa Sokoine, kwenye Mbeya Dabi.

Alipachika bao hilo dakika ya 7 akiwa ndani ya 18 kwenye sare ya kufungana bao 1-1 na Prisons.

Staa mwingine mwenye uwezo wa kupiga mipira mirefu ni beki mkongwe Kelvin Yondan ambaye ni mali ya Geita Gold.