MZAWA Reliats Lusajo ni mtu wa kazikazi kwenye kikosi cha timu hiyo katika mechi za Ligi Kuu Bara ujue umeona pointi kutokana na nyota yake kuwa kali kwenye miguu yake.
Lusajo ni namba moja kwa kutupia akiwa na mabao manne ambayo amefunga kwenye mechi tatu mfululizo alizocheza ndani ya kikosi cha Namungo.
Mchezo wa kwanza ilikuwa Agosti 15,2022, Uwanja wa Mkapa ubao uliposoma Namungo 2-2 Mtibwa Sugar, mabao yote ya Namungo yalifungwa na Lusajo dakika ya 32 na 81.
Pia kwenye mchezo wa pili uliochezwa Uwanja wa Uhuru, ubao ulisoma Ihefu 0-1 Namungo ni yeye alitupia bao dakika ya 50 na bao lake la nne alipachika kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting, ubao wa Uwanja wa Majaliwa uliposoma Namungo 1-0 Ruvu.
Namungo ikiwa imekusanya pointi 7 na kutupia mabao manne ni miguso ya Lusajo imekuwa ya mwisho kwenye kutimiza majukumu yake akishirikiana na wachezaji wengine katika kikosi hicho.
Nyota huyo amesema kuwa kikuwa ni ushindi kwa timu na wanajipanga kwa kila mchezo kupata matokeo.
“Kikubwa ni ushindi kwa ajili ya timu nah ii inatokana na maandalizi mazuri na mbinu ambazo tunapewa na walimu kwenye uwanja wa mazoezi,”.