AZAM FC imefikisha pointi 8 kibindoni na kuwa nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City.
Ni bao la Idris Mbombo ambaye alipachika dakika ya 60 kwenye mchezo huo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Sokoine.
Ni bao la kwanza kwa Mbombo msimu wa 2022/23 ambaye alikamilisha msimu wa 2022/23 alikamilisha kwa kufunga hat trick mbele ya Biashara United.
Unakuwa ni ushindi wa kwanza kwa Azam FC kupata ugenini kwa kuwa mchezo wao wa kwanza waligawana pointi mojamoja dhidi ya Yanga kwa sare ya kufungana mabao 2-2.
Kinara wa ligi ni Yanga mwenye pointi 10 baada ya kushinda mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Ihefu wao wapo nafasi ya 16 wakiwa hawajakusanya pointi kwenye mechi tatu ambazo wamecheza msimu huu wa 2022/23.