LIGI Kuu Tanzania Bara leo Septemba 14 inaendelea kwa timu kusaka pointi tatu muhimu.
Tanzania Prisons wataikaribisha Simba kwenye mchezo wao wa ligi.
Ikumbukwe kwamba Tanzania Prisons ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Mbeya City na Simba ililazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya KMC.
Benjamin Asukile nyota wa Tanzania Prisons ameweka wazi kuwa wanahitaji ushindi kwenye mchezo wa leo.
Nahodha msaidizi wa Simba, Mohamed Hussein ameweka wazi kuwa wanahitaji sapoti ya mashabiki.